MARIAM MANUMBU NYAMWERO
KUZALIWA; Mariamu Manumbu Nyamwero, alizaliwa tarehe 14/06/1961 katika kijiji cha Bunere kata ya Nansimo wilaya ya Bunda mkoa w a Mara. ELIMU; Mariamu Manumbu Nyamwero ,alibahatika kupata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Nambaza mwaka 1969 na kuhitimu elimu ya msingi mwaka 1976. Baada ya kuhitimu Elimu ya msingi alifanya kazi katika kiwanda cha nguo Mutex kilichopo hapa mjini Musoma ,kisha alipata Redandance na akafanya kazi ya secretary katika ofisi ya TRA Musoma mjini. DINI; Mariamu Manumbu Nyamwero,aliamini na alibatizwa mwaka 2014 katika kanisa la Victoria living church. NDOA; Mariamu manumbu nyamwero,aliolewa mwaka 1980 na ndugu .Gervas Mrisho Maganga mkazi wa Musoma Mjini na kubahatika kuzaa watoto 5,wa kiume 4 wakike 1. BIASHARA; Mariamu Manumbu Nyamwero,alijishighulisha na kazi ya ujasiriamali wa biashara ya nafaka kwa muda mrefu hadi umauti unamkuta. UGONJWA; Mariamu Manumbu Nyamwero,alianza kuugua mwaka 2016 ugonjwa wa pressure na kisukari hatimaye ilipofika mwaka 2021 akapata ugonjwa wa kiharusi, aliendelea na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali ikiwemo hospitali ya mkoa wa Mara. KIFO; Marehemu Mariamu Manumbu Nyamwero,alifariki siku ya Jumanne tarehe 28/03/2023 majira ya saa 4 asubuhi akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Mara. FAMILIA; Mariamu Manumbu Nyamwero,ameacha mume na watoto 5,wajukuu26na kitukuu 1. SHUKRANI; Tunashukuru kwa jitihada za madaktari walio kuwa wakimpatia matibabu,ndugu,jamaa na marafiki. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.AMINA.