NEWS ALERT: SHABIKI WA YANGA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

Globu ya Jamii imepokea taarifa ya kifo cha shabiki maarufu wa timu ya Yanga Ally Mohamed almaarufu kwa jina la Ally Yanga.
Taarifa zinaeleza kuwa Ally Yanga amefariki Dunia mapema leo katika ajali ya gari eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin.
UPDATES.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa amethibitisha kifo cha aliyekuwa shabiki maarufu wa klabu ya soka ya Yanga Ally Yanga kilichotokea leo katika ajali ya gari aina ya Rav4 eneo la Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Ally Yanga ambaye pia ni mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya Faidika ambalo lilikuwa kwenye shughuli zake za promosheni na SIO KWAMBA alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.
Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.

Labels: HABARI
posted by prof semeka @ June 20, 2017
0 Comments
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home