UFAHAMU UPUNGUFU WA DAMU : DALILI, CHANZO NA MATIBABU YAKE
Normal = Kiasi cha
kawaida cha damu
Anaemia = Upungufu wa damu (Seli
nyekundu za damu na Haemoglobini huwa kidogo)
Upungufu wa damu ni ile hali
ya kiasi cha damu mwilini kuwa kidogo kuliko kinachotakiwa na mwili kulingana
na hali ya mtu na jinsia yake. Hupimwa maabara na hospitali kwa kuangalia kiasi
cha Haemoglobin, ambayo ni chembechembe za damu na ndiyo hufanya
kazi haswaa za damu kama vile kusafirisha hewa tunayovuta ndani (Oksijeni) na
ile tunayotoa nje (Hewa ya ukaa/Kaboni Dayoksaidi).
Katika hali ya kawaida mwanaume
hutakiwa kuwa na damu kati ya 13.5 hadi 17.5 (gramu za hemoglobini kwa
kila desilita ya damu), na wanawake hutakiwa kuwa na damu kati ya 12.0 hadi
15.5. Tofauti hiyo husadikiwa kwamba huletwa na hedhi ambayo wanawake hupata
kila mwezi na hivyo kuwa na damu pungufu kidogo ukilinganisha na ya wanaume.
Umeelewa? Usihofu. Pole pole
utaelewa na kuwa vizuri zaidi.
Kwa hiyo upungufu wa damu ni ile
hali ya mtu kuwa na kiasi kidogo cha damu (hemoglobini) kuliko kile
kinachotakiwa. Yaani mwanaume kuwa na pungufu ya 13.5 na mwanamke kuwa na
pungufu ya 12.0
Kwa watoto nao pia hutofautiana
kutegemea na umri na jinsia.
SABABU ZA UPUNGUFU WA DAMU
Mambo yafuatayo huweza kusababisha upungufu wa damu
1. Kutokwa na damu nyingi
Hii inaweza kutokana na jeraha au damu nyingi wakati wa
hedhi
2. Magonjwa na Maambukizi
Magonjwa kama vile saratani, seli mundu, magonjwa ya figo,
magonjwa ya ini, magonjwa ya utumbo, minyoo nk huweza kupelekea upungufu wa
damu. Hii ni kwa sababu katika hatua moja au nyingine ya uzalishwaji wake damu
hutegemea urojo wa kwenye mifupa, ini, figo nk. Kukitokea ugonjwa na matatizo
mengine kwenye viungo hivyo basi hata uzalishwaji wa damu utapungua na mtu
kuweza kupata upungufu wa damu
3. Upungufu wa madini ya chuma,
Vitamini B6, Vitamini B12 na Folate
Hizi ndizo malighafi za damu. Ndo vitamini na madini ambayo
hutumika kutengene damu. Hupatikana zaidi kwenye maini, mboga za majani,
matunda, nyama, samaki, mbegu jamii ya karanga na korosho, mayai, vyakula
kutoka baharini, asali, nafaka zisizokobolewa na tende
Endapo mtu hatokula milo kamili na kupata vitamini na madini
hayo kiasi cha kutosha basi anaweza kupata upungufu wa damu.
4. Ujauzito na Kunyonyesha
Wakati wa ujauzito matumizi ya chakula cha mama huongezeka
na virutubisho hugawanywa kati ya mama na mtoto. Endapo mama mjamzito asipokula
vizuri kulingana na hali yake au asipopata virutubisho vya ziada basi anaweza
kupata upungufu wa damu.
5. Baadhi ya dawa
Baadhi ya dawa huweza kuharibu seli za damu au kuingilia
uzalishwaji damu na kupelekea tatizo la upungufu wa damu. Dawa hizo zipo nyingi
sana ila kwa sababu mbalimbali hatutaweza kuorodhesha hapa. Cha msingi ni
kumuulizia daktari na mfamasia wakati unapewa dawa kuhusu athari ya dawa
unazopewa na akujulishe jinsi ya kupunguza au kuzuia athari hizo.
MATIBABU YA UPUNGUFU WA DAMU
Matibabu ya upungufu wa damu hutegemea sana hali ya mtu
mwenye tatizo hilo na kiasi cha damu kilichopungua. Kama hali ya mtu ni mbaya
na kiasi kilichopungua ni kikubwa basi ni lazima aongezewe damu kutoka kwa mtu
mwingine, kama imepungua kidogo na hali ya mtu sio mbaya anaweza kutumia dawa
za kuongeza damu na kupona tatizo hilo.
Cha muhimu zaidi katika matibabu ya tatizo hili ni
kushughulikia chanzo. Kama ni ugonjwa, dawa au tatizo jingine ni vyema
kushughulikiwa chanzo ili mtu akipona aweze kuishi vizuri.
Sambamba na dawa mgonjwa anashauriwa kula vizuri hususan
vyakula vinavyosaidia kuongeza damu.
KINGA DHIDI YA UPUNGUFU WA DAMU
Kwa watu ambao wapo katika hatari ya kupata tatizo la
upungufu wa damu au ambao waliwahi kupata tatizo hili ni vyema zaidi wakajikinga
wasipate tatizo hili.
Kinga bora zaidi ni pamoja na
1.
Kufanya vipimo vya mwili na magonjwa
mengine ambayo yanaweza kusababisha tatizo la upungufu wa damuEndapo
litagundulika tatizo lolote ni vyema litibiwe vizuri na kuendelea na
ufuatiliaji kuhakikisha halisumbui tena
2.
Kula vizuri, kula chakula bora na
milo kamili. Hii ndiyo kinga kuu. Chakula bora ni tiba, chakula bora ni
dawa. Endapo mtu utapata vyakula bora na kula vizuri basi atapata madini na
vitamini za kutosha kuweza kutengezeza kiasi kikubwa cha damu na kumsaidia
asipatwe na upungufu wa damu. Pata madini ya chuma, pata foliki, pata vitamini
B6 na vitamini B12 ya kutosha.
3.
Kutumia virutubisho vya ziada
vinavyosaidia kuongeza damuKwa wenye mahitaji makubwa zaidi basi wanaweza
kujikinga kwa kutumia dawa na virutubisho vinavyosaidia kuongeza damu.Cha
msingi kwenye dawa na virutubisho vya kuongeza damu ni kupima mara kwa mara na
kujua maendeleo yako ili damu isizidi sana. Damu ikipungua ni tatizo, na
ikizidi ni tatizo pia.
Unaweza kuwa na kiasi kidogo cha
damu na ukachelewa kugundua dalili. Anza utamaduni wa kupima kiasi cha damu
angalau mara mbili kwa mwaka. Ukigundua una tatizo anza matibabu haraka na
chukua tahadhali ya kujikinga dhidi ya tatizo hilo
Dalili zifuatazo
zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia
kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya
baadae.
·
Kushindwa kupumua vizuri
·
Vidonda kwenye ulimi au mdomoni
·
Sehemu nyeupe ya jcho kuwa bluu
·
Ngozi kuwa na rangi ya kijivu
·
Kucha kuwa dhaifu
·
Kusikia hasira na kuhamasika haraka
·
Kuchoka sana kuliko kawaida
·
Maumivu makali ya kichwa
·
Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
·
Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama
·
Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
·
Uchovu wa mara kwa mara.
By seleman m Kajana
From Busambara Kibara Bunda- Mara
seremankajana@gmail.com
0766495166/0654006809.
Labels: MAKALA
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home