TAARIFA KWA UMMA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHAGUZI NA UPANGAJI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHAGUZI
NA UPANGAJI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO
CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2017
1.0 UTANGULIZI
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
imekamilisha zoezi la uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kujiunga
na masomo ya Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi vya Serikali kwa
2.0 MATOKEO YA UFAULU KWA UJUMLA
Jumla ya watahiniwa wa shule 349,524 wakiwemo wasichana 178,775 sawa na asilimia 51.1 na wavulana 170,749 sawa na asilimia 48.9 walifanya mtihani wa kumaliza Kidato cha Nne mwaka 2016. Watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo mwaka 2016 walikuwa 47,751wakiwemo wasichana 24,587 sawa na asilimia 51.5 na wavulana 23,164sawa na asilimia 48.5.
Watahiniwa waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018
sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania
Bara. Hivyo ufaulu katika mwaka 2016 uliongezeka kwa asilimia 3.15
ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2015.
2
NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2017
Kwa mujibu wa mwongozo wa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano, mwanafunzi anayeomba kuchaguliwa kuendelea na Elimu ya Sekondari ya Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi hulazimika kujaza fomu ya uchaguzi Selform ambayo ndiyo fomu rasmi ya maombi ya kuchaguliwa. Kwa kutumia fomu hiyo, mwanafunzi hujaza machaguomatano ya tahasusi (Combinations) za masomo anayotaka kusoma na Shule anayoipenda kujiunga nayo kwa kila chaguo.
Kwa kuzingatia utaratibu huo, Mfumo wa kieletroniki wa Uchaguzi hutumika kumpanga mwanafunzi katika machaguo yake ya masomo na Shule kwa kuanzia na chaguo la kwanza hadi la tano kulingana na kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Mfumo humpangia mwanafunzi chaguo la tahasusi aliyofaulu zaidi kuliko machaguo mengine.
Kwa mwaka huu 2017 Uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi umezingatia mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa tarehe 15 Mei, 2017. Mwongozo huu unaelekeza kwamba, kigezo cha mwanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi ni;
i) AAA hadi CCD kama cut off point kwenye masomo ya tahasusi
ii) Credit 3 na pointi zisizopungua 25 kwenye Daraja,
3
iv) Nafasi zilizopo katika Shule husika
Napenda kusisitiza kwamba, vigezo hivi ndivyo vinavyotumika kwa mwanafunzi kujiunga Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka huu. Nia ni kuinua kiwango cha Elimu na Ujuzi kwa Elimu ya Juu Nchini.
4.0 WANAFUNZI WENYE SIFA ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2017
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano mwaka 2017wanatoka kwenye Shule za Serikali na zisizo za Serikali ambapo Shule
351 zikiwemo shule 17 mpya zimepangiwa wanafunzi.
Kati ya wanafunzi 96,018 ni wanafunzi 93,019 ndio wenye sifa za kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama nilivyoainisha hapo juu. Kati ya hao, Wanafunzi 92,998 ni wa Shule (School Candidates) na Wanafunzi 21 walisoma chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
5.0 TAREHE YA KURIPOTI WANAFUNZI KATIKA SHULE
WALIZOPANGIWA
Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa mwaka 2017, utaanza tarehe 17 Julai 2017 lakini kwa wanafunzi wanaongia Kidato cha Sita watafungua Shule tarehe 3/7/2017 kama ilivyokuwa
4
imepangwa. Kwa kuwa upangaji wa wanafunzi wanaoingia Kidato cha Tano kwa mwaka 2017 umezingatia machaguo ya wanafunzi wenyewe na nafasi zilizopo katika Shule husika, hakutakuwa na fursa
ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule.
Nitumie nafasi hii, kuwaagiza wanafunzi wote kuripoti katika Shulewalizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya kufungua Shule , nafasi yake
itachukuliwa na wanafunzi wengine.
6.0 PONGEZI NA SHUKRANI
Napenda kuwapongeza walimu wote kwa juhudi walizozifanya katika ufundishaji na kuwezesha wanafunzi kufaulu vizuri. Hii imetokana na ushirikiano wa walimu, wazazi na walezi katika kuwapatia wanafunzi hao malezi bora.
Aidha, napenda kuwapongeza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi, niwahimize kuendelea kuongeza bidii katika kujifunza ili waweze kufanikiwa kujiunga na mafunzo ya Elimu ya Juu baada ya kuhitimu Kidato cha Sita.
Nawashukuru sana Wadau wote wa Elimu kwa maana ya Viongozi na watendaji wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri pamoja na wananchi kwa ujumla kwa kushiriki kikamilifu kuimarisha Miundombinu ya Shule
5
ikiwemo maabara na majengo mengine muhimu yaliyowezesha Shule kupokea wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa mara ya kwanza.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2017 inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya:

Aidha, fomu za kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi (joining instructions) zinapatikana kwenye shule alikopangiwa mwanafunzi na kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya:
IMETOLEWA NA:
George B. Simbachawene (Mb)
WAZIRI WA NCHI, OR -TAMISEMI.
Labels: HABARI
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home