Friday, 12 January 2018

Kamati Kuu Chadema yapanga kukutana Jumamosi

hadema yapanga kukutana Jumamosi Muungwana Blog 2 Friday, January 12, 2018 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kesho inakutana katika kikao cha ‘dharura’ jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu amesema lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya hali ya kisiasa nchini. Alipotakiwa kueleza kama lengo la kikao hicho ni kujadili ziara ya waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenda Ikulu, Mwalimu amesema kikao hicho si cha dharura kwani kilipangwa kufanyika Desemba mwaka jana lakini kiliahirishwa kutokana na sikukuu za mwisho wa mwaka. Amesema ajenda za kikao hicho zilipangwa kabla Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema hajaenda Ikulu hivyo hakina uhusiano na ziara hiyo ila huenda jambo hilo likajitokeza. “Suala hilo halipo kwenye ajenda ila linaweza kujitokeza na likijitokeza litazungumziwa lisipojitokeza basi,” amesema Mwalimu na kuongeza; “Hata hivyo kwa upande wake inaweza kuwa fursa nzuri kuielezea Kamati Kuu na viongozi wenzake nini kilitokea.”

Labels:

1 Comments:

At 4 March 2022 at 02:21 , Blogger vannagaglio said...

How to get the “Best” slots in casinos by using your
to make use 세종특별자치 출장마사지 of 논산 출장마사지 the best casinos with the best games from and a 성남 출장마사지 bonus 성남 출장안마 in return 당진 출장샵 for your casino.

 

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home